DODOMA JIJI FC YALIMWA FAINI YA MIL. 1 KWA VITENDO VYA IMANI YA KISHIRIKINA

Mechi Namba 213: Dodoma Jiji FC 0-0 Kagera Sugar Fc Klabu ya Dodoma Jiji FC imetozwa faini ya Sh. 1,000,000 (Milioni Moja) kwa kosa la kufanya vitendo vinavyoashiria imani za kishirikina ambapowakati wa mapumziko ya mchezo huo timu ya Kagera ilikuta mlango wachumba chao upo wazi, mayai yakiwa yamevunjwa mlangoni ambapo piachini ulikutwa udi uliochomwa.